Powered by Blogger.
Sunday, November 29, 2015
Saturday, November 28, 2015
WATU WATATU WAUAWA KATIKA SHAMBULIO COLORADO
| Mshambuliaji akiwa ametiwa nguvuni |
Watu 3 wameuawa baada ya kupigwa
risasi na mtu mmoja aliyevamia kituo cha kupanga uzazi katika eneo la
Colorado Springs nchini Marekani.
CHINA KUMALIZA UFUKARA 2020
Shirika la habari
la taifa la Uchina, linasema kuwa viongozi wanamaliza mkutano wa siku
mbili kuhusu namna ya kuondosha umaskini, ifikiapo mwaka wa 2020.
Uchumi
wa Uchina umekuwa haraka katika miongo mitatu iliyopita, na kuwatoa
mamilioni ya watu kwenye umaskini, yaani pato la chini ya dola moja kwa
siku.Lakini watu zaidi ya milioni 70 wa mashambani, bado ni maskini.
Baadhi ya sera za kumaliza umaskini, ni kujenga miji haraka, na kutoa mikopo kwa wakulima wawe wajasiria mali.
Wachambuzi wanasema, kupunguza tofauti kubwa baina ya matajiri na maskini inaonekana kuwa njia ya kuendeleza utulivu
BBC
KOMBE LA CHALLEGE

ETHIOPIA,
Wenyeji wa michuano ya Cecafa maarufu kama chalenji Ethiopia wamejikuta wakilazimishwa sare mbele ya Timu ya Tanzania bara 'Kilimanjaro stars' ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa michuano hiyo, mchuano mkali ulianza kwa Tanzania kujipatia goli wa kwanza kabisa dakika ya 53 kupitia kwa Simon Msuva. Baadaye kabisa dakika ya 90 Ethiopia walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia kujifunga kwa mchezaji wa Tanzania mnamo dakika ya 90
Nao Uganda leo wameibuka kidedea kwa kuifunga Burundi goli 1 kwa sifuri, Uganda ilijipatia goli hilo kupitia kwa Frank kalanda mnamo dakika ya 70 ya mchezo huo
WATATU WAUAWA SHAMBULIO LA ROKETI KASKAZINI MWA MALI
| Wanajeshi wa UN |
MALI,
Watu 3 wamefariki
katika shambulio la roketi katika kambi moja ya vikosi vya kulinda amani
vya Umoja wa Mataifa kaskazini mwa Mali,Umoja wa mataifa umesema.
Wanajeshi wawili wa Umoja huo kutoka Guinea na mjenzi mmoja wameuawa katika shambulio hilo la mji wa Kidal kulingana na maafisa.Ujumbe huo wa kulinda amani nchini Mali uliidhinishwa mwaka 2014 baada ya Ufaransa kuongoza kampeni za kijeshi kuwafurusha wapiganaji wa kiislamu kutoka eneo la Kaskazini.
Jeshi hilo kwa jina Minusma linajumlisha wanajeshi 1000 kutoka mataifa mbali mbali wengi wakiwa ni majirani wa taifa la Mali.
Wapiganaji wa kiislamu wanashukiwa kutekeleza shambulio hilo ambapo watu 14 walijeruhiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa vibaya.
''Kambi yetu ya Kidal ilishambuliwa mapema asubuhi na wapiganaji waliotumia makombora ya roketi'', alisema mmoja wa maafisa kutoka kwa kikosi hicho cha Minusma.
BBC SWAHILI
UTURUKI YAJUTIA KUITUNGUA NDEGE YA URUSI
Urusi-uturuki
Rais wa Uturuki
Rcep Tayyip Erdogan ameonyesha kujuta kwamba Uturuki iliidungua ndege ya
kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wa taifa hilo na Syria,lakini hakuomba
msamaha kwa tukio hilo.
Aliuambia mkutano wa hadhara huko Balikesir kwamba alitamani kwamba tukio hilo halingetokea MWALIMU NYERERE KUPEWA UTAKATIFU
![]() | |||||
| Papa Francis |
Ziara ya Papa Francis nchini Uganda imekuja na sura mpya kabisa na mambo mapya, kwa mujibu wa mtandao wa ETN na pia kwa mujibu wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni kwamba Papa atafanya ziara katika eneo ambalo ni maarufu kabisa kwa wakristo wa barani Afrika kwenda kuhiji.NDANI YA ZIARA YAKE NCHINI UGANDA
Subscribe to:
Comments (Atom)
Recent
Weekly
-
ETHIOPIA, Wenyeji wa michuano ya Cecafa maarufu kama chalenji Ethiopia wamejikuta wakilazimishwa sare mbele ya Timu ya Tanzan...
-
Shirika la habari la taifa la Uchina, linasema kuwa viongozi wanamaliza mkutano ...
-
Mshambuliaji akiwa ametiwa nguvuni Watu 3 wameuawa baada ya kupigwa risasi na mtu mmoja aliyevamia kituo cha kupanga uzazi katika ene...
-
Wanajeshi wa UN MALI, Watu 3 wamefariki katika shambulio la roketi katika kambi...
-
Papa Francis NDANI YA ZIARA YAKE NCHINI UGANDA Ziara ya Papa Francis nchini Uganda imekuja na ...
-
BADO kazi ya kusafisha taasisi za kiserikali inaendelea na imezidi kushika nafasi katika uongozi huu wa awamu ya tano, ikiwa hata mwaka...
-
Urusi-uturuki Rais wa Uturuki Rcep Tayyip Erdogan ameonyesha kujuta kwamba Utur...
