Sunday, November 29, 2015

Saturday, November 28, 2015

CHINA KUMALIZA UFUKARA 2020


 
Shirika la habari la taifa la Uchina, linasema kuwa viongozi wanamaliza mkutano wa siku mbili kuhusu namna ya kuondosha umaskini, ifikiapo mwaka wa 2020.
Uchumi wa Uchina umekuwa haraka katika miongo mitatu iliyopita, na kuwatoa mamilioni ya watu kwenye umaskini, yaani pato la chini ya dola moja kwa siku.

Lakini watu zaidi ya milioni 70 wa mashambani, bado ni maskini.
Baadhi ya sera za kumaliza umaskini, ni kujenga miji haraka, na kutoa mikopo kwa wakulima wawe wajasiria mali.

Wachambuzi wanasema, kupunguza tofauti kubwa baina ya matajiri na maskini inaonekana kuwa njia ya kuendeleza utulivu

BBC

KOMBE LA CHALLEGE

 The official logo for the Council for Easr and Central Africa Football Associations.






ETHIOPIA,
Wenyeji wa michuano ya Cecafa maarufu kama chalenji Ethiopia  wamejikuta wakilazimishwa sare mbele ya Timu ya Tanzania bara 'Kilimanjaro stars' ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa michuano hiyo, mchuano mkali ulianza kwa Tanzania kujipatia goli wa kwanza kabisa dakika ya 53 kupitia kwa Simon Msuva. Baadaye kabisa dakika ya 90 Ethiopia walifanikiwa kusawazisha goli hilo kupitia  kujifunga kwa mchezaji wa Tanzania mnamo dakika ya 90


Nao Uganda leo wameibuka kidedea  kwa kuifunga Burundi goli 1 kwa sifuri, Uganda ilijipatia goli hilo kupitia kwa Frank kalanda mnamo dakika ya 70 ya mchezo huo

WATATU WAUAWA SHAMBULIO LA ROKETI KASKAZINI MWA MALI

Wanajeshi wa UN


MALI,
Watu 3 wamefariki katika shambulio la roketi katika kambi moja ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa kaskazini mwa Mali,Umoja wa mataifa umesema.
Wanajeshi wawili wa Umoja huo kutoka Guinea na mjenzi mmoja wameuawa katika shambulio hilo la mji wa Kidal kulingana na maafisa.
Ujumbe huo wa kulinda amani nchini Mali uliidhinishwa mwaka 2014 baada ya Ufaransa kuongoza kampeni za kijeshi kuwafurusha wapiganaji wa kiislamu kutoka eneo la Kaskazini.
Jeshi hilo kwa jina Minusma linajumlisha wanajeshi 1000 kutoka mataifa mbali mbali wengi wakiwa ni majirani wa taifa la Mali.
Wapiganaji wa kiislamu wanashukiwa kutekeleza shambulio hilo ambapo watu 14 walijeruhiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa vibaya.
''Kambi yetu ya Kidal ilishambuliwa mapema asubuhi na wapiganaji waliotumia makombora ya roketi'', alisema mmoja wa maafisa kutoka kwa kikosi hicho cha Minusma.



BBC SWAHILI

UTURUKI YAJUTIA KUITUNGUA NDEGE YA URUSI

 


Urusi-uturuki
Rais wa Uturuki Rcep Tayyip Erdogan ameonyesha kujuta kwamba Uturuki iliidungua ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wa taifa hilo na Syria,lakini hakuomba msamaha kwa tukio hilo.
Aliuambia mkutano wa hadhara huko Balikesir kwamba alitamani kwamba tukio hilo halingetokea

MWALIMU NYERERE KUPEWA UTAKATIFU


Papa Francis






                                NDANI YA ZIARA YAKE NCHINI UGANDA
 Ziara ya Papa Francis nchini Uganda imekuja na sura mpya kabisa  na mambo mapya, kwa mujibu wa mtandao wa ETN na pia kwa mujibu wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni kwamba Papa atafanya ziara katika eneo ambalo ni maarufu kabisa kwa wakristo wa barani Afrika kwenda kuhiji.

WATATU WAMWAGA UNGA TRA

BADO kazi ya kusafisha taasisi za kiserikali  inaendelea na imezidi kushika nafasi katika uongozi huu wa awamu ya tano, ikiwa hata mwaka haujaisha tangu kuanza awamu mpya ya uongozi. Madudu