Saturday, November 28, 2015

MWALIMU NYERERE KUPEWA UTAKATIFU


Papa Francis






                                NDANI YA ZIARA YAKE NCHINI UGANDA
 Ziara ya Papa Francis nchini Uganda imekuja na sura mpya kabisa  na mambo mapya, kwa mujibu wa mtandao wa ETN na pia kwa mujibu wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni kwamba Papa atafanya ziara katika eneo ambalo ni maarufu kabisa kwa wakristo wa barani Afrika kwenda kuhiji.
Ndani ya eneo la Namugongo ndiyo Papa atafanya ziara na ndani ya ziara hiyo akiwa na lengo la kwenda kumpa utakatifu Baba wa taifa la Tanzania Hayati mwalimu Julius Nyerere kwa kutambua mchango wake mkubwa sana na hata heshima aliyojijengea akiwa kiongozi ndani ya taifa la Tanzanua.

   Namugongo inakumbukwa wazi ni eneo ambalo mashahidi wa dini ya kikiristu waliuawa kwa kuchomwa moto, Papa aliwasilia nchini Uganda jioni saa 4:50 na anatarajiwa kuzuru miji ya Munynyo, Nikiyanja, Nalukolongo na Namugongo kwa siku hii ya leo ambapo atamaliza ziara yake kesho na kuondoka kwenda Afrika ya kati.

  Akiwa anatambua mchango wa Mwalimu Nyerere katika uongozi wake amemua kumpatia utakatifu jambo ambalo limeungwa mkono na watu tofauti wa kidini na kiserikali wa Uganda na hata nchini Tanzania.



“Jukumu la kuendesha mchakato wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa kuwa Mtakatifu ni letu na linaendelea vizuri. Kuna mambo mengi ya kuchunguzwa mpaka mtu kutangazwa kuwa mtakatifu, inawezekana Papa akamzungumzia Mwalimu kwa sababu ya Rais Museveni mara kwa mara ameonyesha kuguswa na mwenendo wa mchakato huo,” alisema Askofu Kilaini.


“Hayati Julius Nyerere alikuwa mwanaharakati wa Afrika ambaye alimpenda Mungu na alijali utu, aliwaunganisha Watanzania wa dini zote na alisaidia ukombozi wa mataifa mengine ya Afrika kama vile Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini na Uganda,” alisema Museveni.
 Naam hao ni baadhi ya viongozi wa kidini na kiserikali waliounga mkono jambo hilo ambalo  ni jambo jingine likiwa limeambatana na ujio wake ndani ya Afrika ya mashariki..
CHANZO: MPEKUZI BLOG




Share this

0 Comment to "MWALIMU NYERERE KUPEWA UTAKATIFU"

Post a Comment