BADO kazi ya kusafisha taasisi za kiserikali inaendelea na imezidi kushika nafasi katika uongozi huu wa awamu ya tano, ikiwa hata mwaka haujaisha tangu kuanza awamu mpya ya uongozi. Madudu mengi ya wafanyakazi wa serikali yamekuwa yakifumbuliwa siku hadi siku, mnamo mapema jana Waziri mkuu Mheshimiwa Majaliwa amefanikiwa kuanika madudu mengi yaliyokuwa yakifanywa hapo bandarini na maafisa wa mamlaka kuu ya mapato yakihusisha ukwepaji kulipaji kodi. Hali hii haikuishia hapo siku hii ya leo imechukua sura mpya kabisa baada ya maafisa watatu wa TRA wamesimamishwa kazi mapema leo. Maafisa hao ambao ni Bw, Angagisye Mtafya, Bw Nsajigwa Mwandengele na Bw Robert Nyoni wamesimamishwa kazi hii leo baada ya uchunguzi dhidi yao kuanza kuchukua nafasi.
Akiongea juu ya suala hilo waziri mkuu amebainisha juu ya uchunguzi wa wafanyakazi kuanza jana ileile, na amemuagiza Kamishna mkuu wa TRA Dkt Philip Mpango kuwaandikia barua wafanyakazi hao.
“Kazi
ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu
wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru
zaidi,” alisema Waziri Mkuu
Pamoja na hayoa maafisa hao hawaruhusiwi kabisa kusafiri kwenda nje ya nchi kama ilivyo kwa Kamishna mkuu aliyefutwa kazi hadi uchunguzi utapakokamilika.
NINI MAONI YAKO JUU YA HILI
0 Comment to "WATATU WAMWAGA UNGA TRA"
Post a Comment