Shirika la habari
la taifa la Uchina, linasema kuwa viongozi wanamaliza mkutano wa siku
mbili kuhusu namna ya kuondosha umaskini, ifikiapo mwaka wa 2020.
Uchumi
wa Uchina umekuwa haraka katika miongo mitatu iliyopita, na kuwatoa
mamilioni ya watu kwenye umaskini, yaani pato la chini ya dola moja kwa
siku.
Lakini watu zaidi ya milioni 70 wa mashambani, bado ni maskini.
Baadhi ya sera za kumaliza umaskini, ni kujenga miji haraka, na kutoa mikopo kwa wakulima wawe wajasiria mali.
Wachambuzi wanasema, kupunguza tofauti kubwa baina ya matajiri na maskini inaonekana kuwa njia ya kuendeleza utulivu
Watu 3 wamefariki
katika shambulio la roketi katika kambi moja ya vikosi vya kulinda amani
vya Umoja wa Mataifa kaskazini mwa Mali,Umoja wa mataifa umesema.
Wanajeshi wawili wa Umoja huo kutoka Guinea na mjenzi mmoja wameuawa katika shambulio hilo la mji wa Kidal kulingana na maafisa.
Ujumbe
huo wa kulinda amani nchini Mali uliidhinishwa mwaka 2014 baada ya
Ufaransa kuongoza kampeni za kijeshi kuwafurusha wapiganaji wa kiislamu
kutoka eneo la Kaskazini.
Jeshi hilo kwa jina Minusma linajumlisha wanajeshi 1000 kutoka mataifa mbali mbali wengi wakiwa ni majirani wa taifa la Mali.
Wapiganaji wa kiislamu wanashukiwa kutekeleza shambulio hilo ambapo watu 14 walijeruhiwa huku watu kadhaa wakijeruhiwa vibaya.
''Kambi
yetu ya Kidal ilishambuliwa mapema asubuhi na wapiganaji waliotumia
makombora ya roketi'', alisema mmoja wa maafisa kutoka kwa kikosi hicho
cha Minusma.
Rais wa Uturuki
Rcep Tayyip Erdogan ameonyesha kujuta kwamba Uturuki iliidungua ndege ya
kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wa taifa hilo na Syria,lakini hakuomba
msamaha kwa tukio hilo.
Aliuambia mkutano wa hadhara huko Balikesir kwamba alitamani kwamba tukio hilo halingetokea